💥💥MUHIMU
Habarini, kuna links za offers mbalimbali zinasambaa sana mtandaoni.
Kama mtaalam wa IT nashauri msizifungue mpaka ujiridhishe.
Hizi links tuwe makini maana endapo utafungua, direct hacker au mhusika akitaka anakuwa na uwezo wakujua mambo yote yanayofanywa kwenye simu au PC/computer yako, na hamna suluhisho mpaka ubadilii device.
Ni hatari na sasa hivi zipo nyingi sana so endapo utapata text ya email au link kama hizo hasa kupitia magrup ya WhatsApp, bora kuuliza kwanza kwa wahusika wa promotion husika.
Kinyume chake, ukifungua tu unakuwa connected na kuanzia hapo mtu anaku-monitor kila kitu unachofanya na sio tu activities za kwenye simu au PC yako bali anaweza hadi akawa anakuona kabisa live unachofanya muda wowote anaotaka.
Anaweza aka-control activities za simu yako mfano kumtumia mtu text/emails kwa kutumia namba yako, kumpigia mtu simu, kufanya miamala mbalimbali ya pesa iwe bank au mitandao ya simu (hii iliwahi kutokea mapema mwaka huu 2021 kwa wateja wa Vodacom waliosmbaziana link ya offer za pesa za bure Tsh 85,000/=),ku-login kwenye akaunti yako yoyote ile unayoijua wewe na akafanya chochote kile (kumbuka unafungua smartphone kwa kutumia email na password).
Yote hii kwa kupitia tu hiyo link utakayo-click inayokuonyesha ofa ya kupewa vitu kama simu sijui hela na kutakiwa usambaze kwenye magrup mengine kwanza.
So kabla ya kufungua kuwa makini kwasababu ukishakuwa hacked ni ngumu kugundua labda tu kama alieku-hack afanye kitu kitakachokushtua moja kwa moja ambacho utaki-notice kupitia notification alert, ila akiamua kufanya vitu vyake kimyakimya,huwezi kujua.
*BAADHI YA NJIA YA HARAKA HARAKA ZA KUJIKINGA*
1. Kabla ya kufungua link yoyote hakikisha unafuatilia kwa umakini hilo jambo kama ni kweli sehemu husika, mfano kuna hiyo link inayoyambazwa kwa kasi sasaivi ikionyesha ofa inatolewa na cocacola, je ni kweli cocacola wametangaza sehemu yoyote katika vyombo vya habari kama ulivyo utaratibu kuhusu hiyo ofa?
Je, umeingia kwenye official website ya cocacola ukaona hiyo ofa imewekwa?
Haya tuseme hujui official website, je, umeingia hata Instagram page yao ukaona kuna tangazo la hiyo ofa?
Kama lipo kweli basi fungua.
lakini kwanini u-click link ambayo haina hata jina la kampuni?
Kwa mfano hiyo link, hapo kwanza haileweki tattyqz ndo kitu gani?
hiyo ni method kwa hackers inaitwa *phishing attack*, hacker anatengeneza link ambayo ndani yake anaweka *codes* ambazo zitaku-monitor na kupata chochote kile anachotaka.
Unaweza ukaona wewe ni kitu kidogo na hakuna kitu cha kuibiwa na hacker lakini fikiria zile namba unazofanya nazo communications kila siku, na wao unawaweka pia kwenye hatari.
For the mean time tuwe tu makini, dunia ya sasa imebadilika sana kiteknolojia
Mtu hakukabi ili umpe hela zako ila unampa wewe mwenyewe tena kiasi chochote anachotaka yeye.
Comments
Post a Comment