Leo nitajaribu kuzungumzia namna au Jinsi ya kuweza ku unlock simu za mitandao mmoja kwa njia ya mkono (cracking)
Na sio kwamba ni simu zote zitakubali njia hii bali ni baadhi ya simu hasa zile zilizokuwa na version 4.4, lollipop na kushuka chini hii ina maanisha kuwa zilizopo juu ya hii nyingi zao huwa zina kataa
Simu hizi ni zile zinazouzwa na mitandao mfano zile simu za promotion za tigo yaani tecno kwani upande mmoja wa line yaani *SIM1* huwa haikubali kusoma line yoyote isipokuwa line ya tigo tu au mtandao husika
*Njia za kuondoa*
Zifuatazo ni njia za kuweza kuondoa tatizo hilo kama utakuwa nalo
Kwanza kabisa download app inayoitwa *MTK Engineering mode* kutoka playstore au unaweza kudownload kupitia link hizi hapa
👇👇
https://m.apkpure.com/mtk-engineering-mode/com.themonsterit.EngineerStarter
https://apkbucket.net/get/apk/1481
links hizo mbili unaweza kutumia kudownlod hiyo app
*Zingatia*
hii ni app ya mtk hivyo basi itakubali kwenye simu zote zenye chipset ya
*Mtk* kama vile tecno
*utaijuaje chipset ya simu yako kuwa ni mtk??*
Pindi utakapo download app hii na kuifungua itakuletea options tatu yaani
*Android settings*
*MTK settings*
*Samsung settings*
Wewe utaingia kwenye *MTK settings* na ikikataa kufunguka basi hiyo simu yako chipset yake sio mtk
Na kama itakubali basi simu yako ni mtk na inabidi tuendelee na process yetu ya ku unlock
Baada ya kuingia kwenye Mtk settings itakupeleka kwenye *Telephony* na hapo utasuka chini mpka sehemu iliyoandikwa *Simme lock*
*Note* pindi utakapoingia kwenye simme lock na ikawa *invisible* yaan rangi yake haijakoza sana na haibonyezeki basi hiyo simu yako itakuwa haikubali process hii
Kwa wale watakao ibonyeza *Simme lock* na kubonyezeka basi hiyo itakubali naitakupeleka mpaka kwenye *SIM1 na SIM2* na hapo utachagua ni upande upi wa line unaotaka ku unlock ila mara nyingi huwa ni SIM1
Baada ya kuchagua upande unaotaka ku unlock utaona sehemu imeandikwa *Network personalization* na baada ya kuibonyeza hii utaingia mpaka *Unlock* na ukishaingia hapa utaambiwa uweke PIN (number) ambazo mimi nimekuwa nikitumia ni *12345678* baada ya kuweka pin hizi utabonyeaza *ok* then utarudi nyuma tena mpaka kwenye *Unlock permanently* then utabonyeza *Finish* na baada ya hapo uta *restart* simu yako na itakuwa tayari kwa kutumia line mbalimbali
📱📱📱📱📱📱
Mpaka kufikia hapo mimi ntakuwa sina la ziada
Ila ningependa kila member wa group hili kujua tricks ndogo ndogo kama hizi kwani kupitia tricks kama hizi nimekuwa nikitengeneza pesa
Na haya ndio mambo tunayotakiwa kufundishana kwani kupitia tricks hizi unaweza kufika mbali
Muhimu zaidi ningependa kukuambia kuwa huu ni muda wako wa kunufaika na smartphone yako sio kutumia muda wako na Mb zako mitandaoni kuangalia mambo yasiokuwa na faida...Asanteni
🙏🙏🙏🙏
Asante
Comments
Post a Comment