Jinsi ya kuzuia udukuzi facebook

JINSI YA KUZUIA MTU KUDUKUA  FACEBOOK YAKO

Sasa kila siku watu wamekuwa wakiulizia jinsi ya ku hack facebook za watu... Kwanini um hack mwenzio?? Huo si wizi kabisa huo 😂😂... Binafsi siwezi kuja kutoa somo kuhusu kum hack mtu facebook yake hiko kitu kwa upande wangu ni upuuzi tu.

Sasa hapa njoeni tuwakomeshe wote wenye mipango ya ku hack facebook za wenzao. Nitatoa njia mbili za kuzuwia mtu ku hack account yako...ya kwanza ya kompyuta na ya pili ya kutumia simu.

Kwa_kutumia_kompyuta

Log in kwenye facebook yako kisha utabofya kimshale kilichopo upande wa juu kulia...kisha baada ya hapo utakwenda kwenye setting kisha utabonyeza security and  log_in iliyoko upande wa kushoto.

Baada ya kufanya hvyo utaona sehemu imeandikwa set_up_two_factor_authentication bofya hapo kisha utabofya neno edit kisha hapo utachagua aina moja ya ulinzi ambayo utapenda kutumia. Lakini kwa ushauri wangu ni vema ukachagua text_message(sms) ambapo kama mtu atakapo taka ku log in kwenye account yako utatumiwa text yenye namba maalumu ambazo ndizo utakazotumia kuingilia facebook.

Kumbuka sehemu hiyo hapi juu haitaweza kufanya kazi kama hujaweka namba yako ya simu hivyo wakati unafanya setting hiyo hapi juu lazma itakutaka kuweka namba zako za simu basi hakikisha unaweka namba zako ndizo zitakazotumiwa kukutumia ujumbe huo mfupi.

Kama tayari umeshaweka namba zako za cm basi utabofya enable kisha utabofya continue bofya tena continue na baada ya hapo utatumiwa code maalumu ambazo Unatakiwa kuziweka kwenye ki boxi maalumu hapo utakuwa tayari umeshawezesha sehemu hiyo. Hivyo basi kila wakati utapotaka ku log in utakuwa unatumiwa code maalumu ambazo utakuwa unaweka kama vile password na ndizo zitakazokuwa zinakuwezesha ku log in.

Kwa_kutumia_simu

Kwa kutumia facebook app log in kisha bofya mistari mitatu iliyoko upande wa kulia juu kisha shuka chini mpaka kwenye account_setting kisha baada ya hapo bonyeza security and log_in kisha shuka chini mpaka ukute sehem imeandikwa use_two_factor_authenticatio  vile vile hapa kama hujaweka namba yako ya simu itakutaka kuweka namba yako kama nlivyoeleza kwa kutumia kompyuta.

Basi kama ulishaweka namba zako za simu bonyeza kitiki kilichopo kwenye kichumba mbele ya neno use_two_factor_authentication kisha utatakiwa kuhakiki account yako kwa kuweka password kisha utabofya continue kisha utatumiwa code maalumu ambazo utatakiwa kuziweka kwenye kibox maalumu kama nlivyoeleza unapotumia kompyuta.

Kwa kufanya hivyo mtu hawezi kuja ku hack account yako kwasababu kila utapokuwa unataka ku log in basi utakuwa unatumiwa code maalumu za kuingiza kama password na huwa zinabadilika kila mara unapotaka ku log in.

Comments

Post a Comment