Fahamu kuhusu airplane mode au flight mode

Airplane Mode ni nini?

```Fahamu matumizi na faida zake```
Mfumo wa Airplane Mode unapatikana kwenye vifaa vingi vya elektroniki kama vile simu janja (smartphones) na hata tableti.
```Je ushawahi jiuliza ni nini
hasa matumizi yake?```
Kwa asili yake ni teknolojia iliyowekwa
kwenye vifaa vya elektroniki kuepusha
muingiliano wa mawasiliano kama vifaa hivyo vikitumika kwenye sehemu kama vile
ndege na sehemu yeyote ambayo haiitajiki muingiliano wa vyombo vya mawasiliano.
Simu au tableti yako ikiwekwa kwenye mfumo wa Airplane Mode utaweza kugundua kupitia kialama cha ndege irukayo kinachokuwepo
katika eneo la ‘Notifications’.(yaani alama hii)
Airplane Mode inasaidia kuzima
teknolojia ya mawasiliano ya –
kiredio (mjumuisho wa Bluetooth,
WiFi na mitandao ya simu) kwa njia
rahisi ya kuchagua eneo moja tuu.
Kitendo cha kuweka Airplane mode
kitasaidia ata kufanya simu au tableti yako
kudumu muda mrefu zaidi na chaji ingawa
hili litafanikiwa kutokana na huduma nyingi
kuzimwa.
>Celullar: Mfumo wa mawasiliano ya
simu kupitia laini yako huzimwa.
Hii inamaanisha huduma za kupiga na kupokea simu, ujumbe wa SMS na huduma
ya intaneti (data) kupitia mtandao wako
wa simu huzimwa pia.
>WiFi:huzimwa pia.
Huduma ya intaneti kupitia mfumo wa WiFi huzimwa pia. Ingawa kwa baadhi ya vifaa vya kisasa zaidi bado unaweza kuwasha
huduma ya WiFi baada ya kuweka Airplane
Mode.
>Bluetooth:Utumiaji wa Airplane Mode huzima pia
huduma za bluetooth.
>GPS:huzimwa pia
GPS ni moja ya teknolojia muhimu kwa
simu za kisasa inayotumiwa na apps nyingi
kuweza kutambua masuala ya kijiografia
kuweza kutambua kifaa chako kipo eneo
gani duniani.

                           Je kuna faida gani ya kutumia Airplane Mode?
 
Kwenye baadhi ya maeneo hakuna ruhusa
ya watu kuweza kutumia vifaa vya
mawasiliano vinavyoweza kuingiliana na
mfumo mwingine wa kimawasiliano, mfano
kwenye ndege.
Teknolojia hii imerahisisha watu wenye
vifaa vya elektroniki kuweza kuvitumia ata
pale wakiwa kwenye ndege kama tuu
wakihakikisha vifaa hivyo vimewekwa
kwenye Airplane Mode.
Inasemekana muda wote simu
zinatuma signal kutafuta mnara wa
mawasiliano na kama ndege yenye
abiria wengi ndani yake na wote
wakiacha simu zao zikiwa zimewaka
basi itapokuwa hewani simu hizo zote
zitakuwa zinatuma signal nyingi za
kutafuta mawasiliano na hili linaweza
ingiliana na mfumo wa mawasiliano
wa ndege na hili linaweza leta tatizo
kwa rubani katika ufanisi wake.
Pia faida kuu inaweza ikawa kwenye
kukusaidia kuendelea kutumia kifaa chako
kwa kazi zingine bila utumiaji mwingi wa
chaji. Hii ni kwenye simu, tableti na ata
baadhi ya laptop.
Kumbuka mara zote kifaa chako
kinapokuwa kimeweka basi kuna
mifumo mingi ya kimawasiliano ya
kiredio – yaani mtandao wa simu,
bluetooth, wifi na GPS huwa
vinafanya kazi inayotumia kiwango
kikubwa cha chaji.
Baadhi ya vifaa vinaruhusu WiFi na
Bluetooth kufanya kazi ata vikiwa kwenye
Airplane Mode.
Baadhi ya vifaa vya kisasa zaidi vinaruhusu
baada ya kuweka kifaa chako kwenye
Airplane Mode utaweza kuwasha na
kutumia huduma za WiFi au Bluetooth.
Hii ni kwa sababu kwa siku hizi kuna hadi
ndege zinazotoa huduma ya WiFi ndani
yake, zina teknolojia kubwa ya kusaidia
kuepusha teknolojia hiyo kuingiliana na
teknolojia za kimawasiliano za ndege.
Je huwa unaitumia teknolojia ya
Airplane Mode? Na katika hali gani
unajikuta unatumia teknolojia

Comments