Je wajua kubadili stock rom (kuflash)?

JINSI YA KUBADILI STOCK ROM YA SIMU ZA TECNO

Post hii haina lengo la kuwa haribia watu biashara zao  hasa wale mafundi simu wanaojihusisha na ku flash simu😂😂. Tunajifunza tu

#ku_flash_simu_ni_nini??

Hili ni neno linalutimiwa na mafundi au kiufundi likiwa na maana kwamba kurudisha au ku repair mfumo au sehemu ya mfumo wa uendeshaji kwa ku install copy ya mfumo huo ili kufanya simu yako kufanya kazi kama inavyotakiwa.

#mahitaji_muhimu

👉unatakiwa kuwa na USB data cable

👉MT6577 USB VCOM drivers
(win 7/8 na vista download kupitia hyo link hapo mbele)....  Hapa

👉SP flash tool
( download kupitia hyo link hapo mbele)....  Hapa

👉Rom za tecno
( download kupitia link hiyo hapo mbele... Hakikisha una download room kutokana na jina la simu yako)...  Hapa

👉kompyuta... Iwe laptop au desktop whatever

#HATUA

1. Zima simu yako na utoe betri ila kama simu yako ina betri la ndani moja kwa moja basi hakikisha simu yako imezima kabisa yani.

2. Fungua program ya SP flash ambayo umedownload kupitia link hapo juu.

3. Fungua folder yenye program hiyo kisha chagua #SP_flash_tool.exe kisha bofya kitufe cha kulia kwenye mouse yako kisha bofya #Run_as_administrator

4. Kisha baada ya program hiyo kufunguka bonyeza mahali palipoandikwa #scatterLoading iliyopo upande wa kulia chini kidgo.

5. Baada ya hapo chagua mahali ulipo hifadhi ROM ya simu yako baada ya ku download kisha chagua file hilo na bofya open... Kumbuka mara nyingi file hili linakuwa na mfumo wa text mfano ( MT6577_android_scatter_emmc.txt) hivyo kumbuka kuchagua file linaloendana na simu yako ukikosea tu utaharibu simu yako.

6. Weka tiki kwenye vyumba vyoote isopokuwa chumba kilichoandikwa #PreLoader na #DSP_BL.. Pia hapo ni vema kuwa makini sana maana unaweza kuharibu simu yako.

7. Baada ya hapo toa betri la simu yako kama umesahau na kwa wale ambao simu zao zina betri kwa ndani basi hakikisha imezima kabisa kisha sasa bonyeza #YES kwenye program ya #SP_Flash_tool.exe

8. Kwa haraka kabisa chomeka simu yako data cable kisha bofya vibonyezeo vyote vya sauti ( yani cha kupandisha saut na cha kushusha sauti ) pamoja na cha kuzimia simu.

Baada ya kufata mtiririko wote huo kwa makini kabisa utaona simu yako ikianza kupokea files kutoka kwenye kompyuta... Subir mpaka imalize na kama umefata hatua zote vzur bas utaona message inayosema #you_have_successful_restored_the_stock_ROM.

Basi ndo nikawa nimemaliza hvyo na endapo utakosea hatua hizo na kuharibu simu yako basi mtoa post na post hii havitahusika kwa namna yoyote ile.

Comments