Satelaiti.

MAWASILIANO YA SATELAITI
Satelaiti ni nini?
Nikifaa (au mtambo) ambao huwekwa angani kuzunguka dunia au kitu chochote kilichoko angani.

Satelaiti ya kwanza kutengenezwa na binadamu, kupelekwa angani na kuwekwa katika obiti kuzunguka dunia iliitwa SPUTNIK 1. Ilitengenezwa na Urusi na kupelekwa angani tarehe 4 Octoba, 1957. Satelaiti hii ilisafiri kwa mwendo wa kilomita 29,000(km) kwa saa ikitumia dakika 96.2 kukamilisha mzunguko wa dunia. Ikiwa angani ilituma mawimbi ya mawasiliano katika masafa ya 20.002MHz na 40.002MHz ambayo yalipokelewa na mitambo ya redio za amateur “amateur radio” duniani kote.

Kuna satelaiti za aina mbili:
1. Satelaiti za asili (Natural satellites) mfano; Dunia na Mwezi
2. Satelaiti za kutengenezwa na Binadamu (Artificial satellites).

Kuna aina ngapi za Satelaiti za kutengenezwa na binadamu?
Zipo satelaiti za aina nyingi na zimetengwa kwa matumizi mbalimbali.
   > Satelaiti kwa ajili ya utafiti na uchunguzi sayari za mbali, galaxies na vitu vingine vinavyoelea angani ( Astronomical satellites ).
  > Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufanya mawasiliano ( Communications Satellites).
  >Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kuangalia hali ya hewa ( Weather Satellites).
  > Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya matumizi ya Ki-intelijensia na Kijeshi (Intelligence
and Military Operations Satellites ).
  > Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufanya utafiti wa dunia na vitu vingine vilivyoko angani mfano ( Biosatellites ambazo hubeba viumbe hai kwenda angani kwa ajili ya utafiti).
   > Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufuatilia mabadiliko ya dunia na mazingira ( Earth
Observational Satellites).
   > Ofisi za uchunguzi wa anga zinazoelea angani ( Space Stations ).
   > Vifaa (mitambo) vyote vinavyokuwa angani katika obiti ( Manned Spacecrafts / Spaceships).
  >Satelaiti ndogo zinazounganishwa katika satelaiti nyingine kwa waya mwembamba unaoitwa tether ( Tether Satellites)
  > Satelaiti kwa ajili ya kutambua (mahali/ sehemu) katika uso wa dunia (positioning satellites) mfano
Glonass ni mfumo wa Urusi, GPS (Global Positioning System) ni mfumo wa Marekani, GALILEO ni mfumo wa Ulaya (European Union), China mfumo wao COMPASS kwa sasa unaitwa BeiDou, IRNSS ni mfumo wa India. Mfumo wa
GNSS (Global Navigation Satellite System) huunganisha mifumo niliyoitaja hapo juu.
Satelaiti zote hapo juu zipo katika obiti (orbit) zilizopo katika umbali tofauti kutoka katika uso wa dunia. Obiti hizo ni:
LEO (Low Earth Orbit) umbali kuanzia kilomita 0 hadi 2000km juu ya uso wa dunia; baadhi ya satelaiti zilizopo katika ukanda huu ni Kituo cha Kimataifa cha Satelaiti kilichopo umbali wa kilomita mia nne (400km) kutoka katika uso wa dunia kinachoitwa ISS ( International Space Station ), satelaiti za uchunguzi wa dunia ( earth observation satellites ), satelaiti za upelelezi, Satelaiti zinazotumika katika " Remote Sensing"
KITUO CHA KIMATAIFA CHA SATELAITI ( INTERNATIONAL SPACE STATION - ISS) KINACHOZUNGUKA DUNIA KATIKA OBITI AMBAYO IPO UMBALI WA KILOMITA 400km (kinaelea kati ya 330km na 435km kutoka ardhini) KUTOKA ARDHINI.
Taarifa nyingine:
Kilirushwa angani tarehe 20 Novemba, 1998
Kinazunguka kwa kasi ya 7.66km/s katika obiti ambapo kasi yake ya juu kabisa (Max Speed) ni 27,600km/saa.
Kiligharimu dola za Kimarekani Bilioni 150 (150 Billion Us Dollar).
Kina sehemu mbili Sehemu ya Urusi (Russian Orbital Segment) na Sehemu ya Marekani (United States Orbital Segment).
MEO/ICO (Medium Earth Orbit/Intermediate Circular Orbit) umbali kati ya kilomita 2000km na 35786km juu ya uso wa dunia; baadhi ya satelaiti zilizopo katika ukanda huu ni satelaiti za utambuzi wa mahali katika uso wa dunia namaanisha za GPS (kilomita 20,200km), GLONAS (19,100km), GALILEO (23,222km), satelaiti zinazotumika kutuma na kupokea mawasiliano kaskazini mwa dunia (northern pole) na kusini mwa dunia (southern pole).
MIFUMO MBALIMBALI YA SATELAITI
GEO (Geostationary Earth Orbit) : Umbali wa kilomita 35,786km juu ya uso wa dunia katika Ikweta. Satelaiti zilizopo katika umbali huu huzunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia.
Mfano wa satelaiti zilizopo katika umbali huu ni zile za mawasiliano ya Televisheni, Data (intaneti), redio, mawasiliano ya simu ( mfano Thuraya ambayo hutumia satelaiti mbili ambazo ni Thuraya 2 na Thuraya 3 ambazo hutumika kutoa huduma za mawasiliano ya simu za satelaiti "satellite phones" katika bara la Asia, Afrika, Ulaya na Australia ), mawasiliano ya kiintelijensia, mawasiliano ya kijeshi, satelaiti za uchunguzi wa hali ya hewa, satelaiti za kurekebisha data katika uso wa dunia ( mfano OmniSTAR ).
Nukuu > Satelaiti zote zilizopo katika umbali wa kilomita 35,786km juu ya uso wa dunia katika Ikweta (latitudo 0) huzunguka sawa na kasi ya dunia. Satelaiti zilizopo katika umbali huo juu ya uso wa dunia nje ya mstari wa Ikweta haziwezi kuzunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia.
HEO (High Earth Orbit) : umbali zaidi ya kilomita 35,786km. Satelaiti zilizopo katika umbali huu huzunguka kwa kasi ndogo kuliko kasi ya dunia. Mfano wa satelaiti iliyoko katika ukanda huu ni vela 1a
Satelaiti tunazozitumia kupokea mawimbi ya televisheni / redio zipo katika kundi la Satelaiti za Mawasiliano (Communication Satellites).
Satelaiti hizi za mawasiliano tunazozitumia kupitisha mawasiliano ya televisheni na redio (zipo katika Geosynchronous Orbit) umbali wa kilomita 35,786km kutoka ardhini katika Ikweta na husafiri kwa kasi sawa na kasi ya dunia.
Mawasiliano kutoka katika satelaiti za mawasiliano zilizopo katika "Geosynchronous Orbit"(GSO).

Jinsi ya kutafuta channel za tv na station  za radio kwa kutumia satelite mbalimbali
Kwa kuwa dunia ina umbo la duara si rahisi watu wote tulioopo katika uso wa dunia (namaanisha mabara yote) tukatumia satelaiti moja kupokea mawasiliano toka katika satelaiti. Kusema hivi namaanisha mfano satelaiti tunayoitumia sana (IS 906 @ 64.2E (nyuzi za longitudo 64.2 Mashariki mwa Greenwich) katika ukanda wetu Tanzania ikiwemo haiwezi kufikisha mawimbi yake Marekani kwa sababu Marekani wanakuwa upande mwingine wa uso wa dunia (they are below the horizon of the reach of this satellite) hii ni vile vile kwa satelaiti zinazoimulika Marekani hata sisi hatuwezi kupata mawimbi yake. Mfano baadhi ya satelaiti za Intelsat (IS 902, IS 906, IS 904, IS 10, IS 17, IS 907 na nyinginezo zilizoko juu ya usawa wa Afrika na bahari ya Hindi na wao wakitaka kupokea mawasiliano yake wanatumia kituo chao kilichopo Afrika Kusini au vituo vingine.

Baadhi ya satelaiti ambazo nilishazifanyia utafiti na mawimbi yake yanafika hapa Tanzania zipo kati ya nyuzi za longitudo 27 Magharibi mwa Mstari wa Greenwich na nyuzi za longitudo 85 Mashariki mwa Mstari wa Greenwich. Dishi linalozunguka (horizon to horizon) linaweza kupata chaneli mbalimbali kutoka satelaiti hizi kwa kuzunguka kupitia satelaiti moja baada ya nyingine (from 27 West to 85 East). Kadri unavyoelekea Magharibi ya dunia ndivyo utakavyozidi kupata satelaiti zilizopo Magharibi ya dunia huku ukipoteza za Mashariki ya dunia; na kinyume chake (and vice versa).
Baadhi ya satelaiti ambazo zinazunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia; ambazo zipo katika "Geosynchronous Orbit or Parking Orbit" zinazopatikana katika eneo letu (Tanzania na nchi za jirani zimeorodheshwa chini. Satelaiti hizi hutumika kwa mawasiliano mbalimbali mfano Data /Internet, Televisheni, Radio, Mawasiliano ya Ki-intelijensia, kijeshi na mawasiliano mengine.

Intelsat 907 @ 27.5W: VoA TV, Alhurra TV Iraq, Alhurra TV Europe, RTG (Guinea),
Intelsat 905 @ 24.5W: Nile Drama, Syria 1,
SES 4 @ 22W: Bolivia Mux, Truth TV, TV Universal,

NSS7 @ 20W: CNN, TBN, Emmanuel TV, MBC (Malawi), Lesotho TV, TPA, Trinity Broadcasting

Intelsat 901 @ 18W : Ethiopia Educational Media Agency
Telstar 12 @ 15W:

Nilesat 201 @ 7W: DW Arabia, BBC Arabic, Abu Dhabi, Abu Dhabi Sport 1, Dubai Sport 2, DM, TV, National Geographic Channel,

Intelsat 10 - 10W @ 1W: BBC World Service, RTS1 (Senegal)
Rascom QAF 1R @ 2.8E: Libya Satellite TV, Libyan Mux, RTNC, Digital Congo (Congo)
SES 5 @ 5E: ZUKU , SABC 1, SABC 2, SABC 3, ETV, STARTIMES

Eutelsat 7A @ 7E: Record Mozambique, MBC 1, MBC 2, CRTV, RTS 1 (Senegal), BBC Persian, ORTM, Raha Tv, TPA Internacional, VoA TV Persian, Azam TV,

Eutelsat 10A @ 10E: Startimes, Agape TV Network,
Amos 5 @ 17E: Zambia Mux, Reuters Live, Doordarshan, Kingdom Africa TV, Bible Exploration TV, Fashion TV Europe, TING (Tanzania), Continental, (Amos 5@ 17E ilipoteza mawasiliano na ardhini (duniani) tarehe 22/11/2015).

Eutelsat 36A @ 36E: TING Channels (Tanzania), NTV Plus, Afrique TV,
Eutelsat 36B @ 36E: CCTV News, CCTV 4 Europe,

Multichoice DStv channels
NSS 12 @ 57E: ZUKU , KBC- Kenya , Family TV - Kenya, ETV (Ethiopia), VoA TV Africa, American Embassy tv Network etc.),

Intelsat 904 @ 60E: Uganda Mux, Kenya Mux, NTV (Kenya), KBC Channel 1 (Kenya), TBC 1, NTV, Uganda (Kenya), Swazi TV, ZNBC,

Intelsat 902 @ 62E: NTV (Kenya), Citizen TV (Kenya), SABC 1 - 3 (South Africa), Sky International,
Intelsat 906 @ 64.2E: ITV, EATV, CAPITAL, TBC, STARTV, TVM (Mozambique), UBC (Uganda), Chanel 10,

Hayo machache kutoka vyanzo mbali mbali....

Comments